LILIAN ODIRA AWEKA REKODI MPYA KWENYE MASHINDANO YA DUNIA
Lilian Odira ameishangaza Dunia kwa kutoka nyumba na kutwaa ubingwa wa mbio za mita 800 kwenye Mashindano ya Dunia.
LILIAN ODIRA ndiye bingwa wa mbio za mita 800 upande wa wanawake na ameweka rekodi mpya kwenye mashindano haya ya Dunia ambayo yatafikia kikomo leo Tokyo nchini Japan. Odira ambaye alikuwa anapigiwa debe kufanya vyema kwenye mashindano haya amewaacha wengi vichwa wazi baada ya kukimbia muda wa dakika 1:54.62.
Odira aliwashinda Georgia Hunter Bell wa Great Britain ambaye alimaliza wa pili na muda wa dakika 1:54.90 huku Keely Hodgkinson wa Great Britain akimaliza wa tatu na muda wa dakika 1:54.91. Wakenya wengine Sarah Moraa na Mary Moraa walimaliza nafasi ya 4 na 7 mtawalia.
Hii ilikuwa ni dhahabu ya 7 ya Kenya kwenye mashindano haya na ya 5 kutoka kwa kikosi cha wanawake ambao walituwakilisha kwenye mashindano haya. Kina dada walishinda dhahabu kwenye mbio za mita 800, 1500, 3,000, 5,000, 10,000 na mbio za kilomita 42.
Je, Una Hisia Gani?
Penda
0
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0