NANI ATAKUWA BINGWA WA FKF PREMIER LEAGUE 2025/2026?

MSIMU MPYA LIGI KUU NCHINI UMEANZA RASMI, NANI ANA MAKALI YA KUTESA?

Sep 20, 2025 - 17:58
Sep 20, 2025 - 18:03
 0  10
NANI ATAKUWA BINGWA WA FKF PREMIER LEAGUE 2025/2026?
Mechi ya Ligi Kuu nchini

Ligi bora duniani FKF Premier League ilianza rasmi jana. Kimekuwa kipindi kigumu kwa wapenzi wa soka wa klabu za Ligi Kuuigi Kuu Nchini lakini sasa subira yao hio imevuta heri tumbo zao zimeacha kuumia kwa kuwa ngoja ngoja haipo tena.

Timu 18 zitashiriki Ligi msimu huu. APS Bomet kutoka kaunti ya Bomet watakuwa wanashiriki Ligi Kuu msimu huu kwa mara ya kwanza kabisa8 kwenye historia hii baada ya kumaliza nafasi ya pili kupandishwa daraja kutoka National Super League msimu uliopita. Timu nyingine ambayo itashiri Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ni Nairobi United maarufu Naibois yenye makao yake jijini Nairobi ambao walikuwa mabingwa wa National Super League msimu uliopita.

Msimu huu bingwa wa FKF Premier League atapokea kitita cha Shilingi Milioni 15, nafasi ya pili atapokea milioni 3 huku nafasi ya tatu akienda nyumbani na shilingi milioni 2. Tumeshuhudia kuongezeka kwa hela ambazo bingwa wa Ligi Kuu anapokea tofauti na msimu uliopita ambapo mshindi alikuwa anapokea Milioni 2.

Kuongezeka kwa hela hizi kutachangia msisimko wa Ligi na tutashuhudia timu zikijituma zaidi. Kenya Police FC ambao ndio bingwa mtetezi wa mashindano haya wanataka kutetea ubingwa wao msimu huu swali ambalo wengi wanajiuliza watatoboa? Gor Mahia wana hasira ya kutoka mikono mikavu msimu uliopita wamefanya sajili nzuri kabla ya msimu mpya kuanza, wana kocha mpya Charles C.K Akonnor raia wa Ghana ambaye amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana The Black Stars, unadhani atakuwa na ushawishi wa kuwafanya Sirkal kupata taji msimu huu? AFC Leopards wana kiu ya miaka 27 bila kushinda taji la Ligi Kuu, Chini ya uongozi mpya wa Mwenyekiti Bonface Ambani unadhani watakuwa na mwamko mpya? Kakamega Homeboyz nao wamekuwa wakinusia tu mwaka huu itakuwa hivo tena ama hii ni zamu ya Shabana ambao wamekuwa wakisuka kikosi chao kutoka msimu uliopita na sasa wanasema wako tayari kabisa kupambania ubingwa msimu huu. Wengine wanaopigiwa debe kutwaa ubingwa ni KCB na Tusker FC. 

Bingwa wa FKF Premier League atakuwa nani?

Je, Una Hisia Gani?

Penda Penda 0
Sipendi Sipendi 0
Penda Penda 0
Ya Kufurahisha Ya Kufurahisha 0
Mwenye hasira Mwenye hasira 0
Huzuni Huzuni 0
Lo! Lo! 0