AFCON 2025- SENEGAL WAZUA MALALAMISHI

Shirikisho la soka nchini Senegal kimetoa malalamishi kuwa wanachezewa mchezo mbaya na Morocco kuelekea fainali yao hapo kesho.

Jan 17, 2026 - 14:44
Jan 17, 2026 - 14:45
 0  15
AFCON 2025- SENEGAL WAZUA MALALAMISHI
Wachezaji wa Senegal wakisherekea kwenya mchuano wao wa awali.

Senegal wametoa malalamishi ya shirikisho la soka barani Afrika CAF kabla ya mchuano wa kukata na shoka wa fainali baina yao na Morocco jijini Rabat.  
Kati ya vitu ambavyo Senegal wanalalamikia ni:

Uwanja wa mazoezi:

Teranga Lions wamekataa kuutumia uwanja wa Mohammed VI Football Complex, kwani uwanja huo uko karibu na hoteli ambayo kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kinapokaa. Wanahisi kuwa mpinzani wao anaweza akafuatilia mazoezi yao kurekodi. Wameiomba CAF kuwapa uwanja mwingine wa mazoezi. 

Mauzo ya tiketi: 

Senegal wamelalama vikali kuwa mwenyeji Morocco anafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa mashabiki wao wanakosa tiketi licha ya kuwa na idadi kubwa ya mashabiki wa Senegal ambao wako Morocco kwa sasa ambao wanataka kuja kuwashabikia hapo kesho. 

Licha ya chamgamoto hizo wamefanikiwa kupata:

* Tiketi 300 – Kategoria 1
* Tiketi 850  – Kategoria 2
* Tiketi  1,700  – Kategoria 

Usalama: 
Senegal wanasisitiza kuwa usalama wa wachezaji wao pindi walipotua Rabat, ulikuwa wa kutilia shaka na kuwaacha mashabiki kutangamana na wachezaji bila hatua za usalama kuchukuliwa imewapa wasiwasi. Ikumbukwe kuwa Morocco ndio wenyeji wa AFCON 2025 na wanafanya kila wawezalo kutwaa ubingwa huu. Mara ya mwisho walinyakua taji hili ilikuwa ni 1976. 

Unadhani mbini hizi za unyanyasaji zitawapa taji? 

#AFCON205  #Senegal #Morocco

Je, Una Hisia Gani?

Penda Penda 0
Sipendi Sipendi 0
Penda Penda 0
Ya Kufurahisha Ya Kufurahisha 0
Mwenye hasira Mwenye hasira 0
Huzuni Huzuni 0
Lo! Lo! 0