KENYA ITAZIMA NDOTO YA IVORY COAST?
Huu ni mchuano wa mwisho hatua ya makundi ya kufuzu Dimba la Dunia unadhani Kenya atakuwa mkosi kwa Ivory Coast?
Hapa ni mchuano wa kufa kupona, ni ndoto ambayo kila taifa iko nayo kufuzu dimba la Dunia na hii itakuwa wazi Stade Olympique Alassane Ouattara wakati Ivory Coast watakuwa wakijaribu kuuhepa mtego wa Benii McCarthy na kikosi chake. Hapa Kenya anajua wazi kabisa hana nafasi ya kufuzu ila kwa Ivory Coast ni mchuano ambao lazima washinde kivyovyote vile wanahitaji hizi alama tatu.
Japo kuwa wanaongoza kundi F ambalo lina Gabon, Gambia, Seychelles,Burundi pamoja na Kenya ni alama 1 tu inawatofautisha na Gabon ambao wako nafasi ya pili na wana nafasi ya kufuzu iwapo watashinda na Ivory Coast washindwe kuipiga Kenya.
Africa ya majina makubwa kucheza soka iliisha Africa ya sasa mpira ni dakika 90 na majina makubwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kama vile Simon Adingra anayechezea Sunderland, Sebastian Haller wa Dortmund, Amad Diallo wa Manchester United kutaja tu wachache hawatakuwa tishio kubwa kwa Kenya kwani mechi ya mkobdo wa kwanza tulitoka sare ya kutofungana.
Nani atabeba alama 3 muhimu baada ya dakika 90?
Je, Una Hisia Gani?
Penda
1
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0