CAMEROON YA MIKOSI, USIMGUZE UKITAKA KUSHINDA AFCON.
Kila ambaye amekuwa akikuta na Cameroon ameambulia patumu kwenye fainali. Bahati mbaya tu ama Cameroon ina mikosi?
AFCON 2025 ilitamatika rasmi hapo jana na kumekuwa na stori kibao kuhusi mashindano na ya mwaka huu nanwengi walitarajia mwenyeji Morocco atakuwa bingwa wa mwaka huu. Hilo sio kweli Senegal maarifu kama The Teranga Lions ndio mabingwa wa AFCON 2025. Hongera sana kwao.
Ukiachia sasa na mambo ya ubingwa, wengi wanasema kuwa The Indomitable Lionsya Cameroon ni kama wana mkosi mbaya sana kwenye mashindano haya. Damu yao huezi ukaipeleka kwa mganga na hata ukifanikiwa kuipeleka itakuletea madhara.
Mwaka huu nchini Morocco, huyu mwenyeji Morocco ambaye alikuwa anapigiwa debe kutwaa ubingwa alimwondoa Cameroon kwenye hatua ya robo fainali na jana mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani alishindwa kukata kiu ya zaidi ya miaka 50 na akanyimwa taji na Senegal.
Mwaka jana nchini Ivory Coast kwenye AFCON 2023 Nigeria walimbandua Cameroon na wakapoteza kwenye fainali hio dhidi ya mwenyeji Ivory Coast ambao walikuwa mabingwa.
2021 nchini Cameroon, Egypt waliwaondoa wenyeji Cameroon na wakapoteza fainali hio dhidi ya Senegal. Yaani ukitaka kushinda AFCON Cameroon ni mkosi mbaya kabisa ukimwondoa tu, mambo yako yatakuwa magumu. Ukitaka kushinda AFCON usimguze Cameroon.
Unaamini kwenye huu mkosi wa Cameroon?
Je, Una Hisia Gani?
Penda
2
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0