EMMANUEL WANYONYI AMEVUNJA REKODI YA MASHINDANO YA DUNIA.
Emmanuel Wanyonyi amevunja rekodi ya mbio za World Athletics Champions nchini Japan
Emmanuel Wanyonyi ameshinda mbio za mita 800 kwenye mashindano ya World athletics Championship Tokyo, nchini Japan. Wanyonyi ametumia muda wa dakika 1:41.86 na kuweka rekodi mpya ya mashindano hayo. Mkimbiaji huyo ambaye pia ni bingwa wa mashindano ya Olimpiki alitumia mbinu tofauti leo, alianza kwa kuongoza wakiambiaji wenzake na akasalia uongozini hadi dakika ya mwisho.
Ameshuhudia ushindani mkubwa kutoka kwa sDjamel Sedjati wa Algeria ambaye alimaliza nafasi ya pili kwa kukimbia muda wa dakika 1:41.90 na Marco Arop wa Canada ambaye amekimbia muda wa dakida 1.41.95.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutwaa ubingwa Wanyonyi anasema kuwa lengo lake kuu ilikuwa ni kushinda dhahabu na alikuwa tayari kujitoa kivyovyote vile. " Nilikutana na David Rudisha jana kabla ya pambano na akanieleza kuwa nipumzike vizuri na nijipe tumaini kuwa kila kitu kinawezekana" - aliongezea Wanyonyi.
Je, Una Hisia Gani?
Penda
0
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0