AUSTIN ODHIAMBO- KENYA TUKO TAYARI KABISA
Kiungo mbunifu wa Harambee Stars amesema kuwa wako tayari kabisa kuipambania nchi yao.
Kiungo mbunifu wa Harambee Stars AUSTIN ODHIAMBO amezungumzia kuhusu maandalizi ya kikosi hicho na amesema kuwa Kenya iko tayari kabisa kwa mashindano haya ya CHAN ambayo yameng'oa rasmi leo nchini Tanzania. Odhiambo anasema kuwa mafunzo ambayo wamepata ni dhihirisho tosha kuwa kila kitu kipo shwari kambini.
“Ingekuwa uwezo wangu ningeta hata mchuano wetu dhidi ya DRC ukuwe leo.”
Austin amezungumza na waandishi wa habari na amesema kuwa kama Kenya wanataka kupiga hatua zaidi kwenye mashindano haya wanafaa kushikamana. Anaamini kuwa hakuna timu ngumu ikiwa kikosi chao kitacheza kwa umoja na kuwa na malengo sawa. Amemsifu mkufunzi Benny McCarthy kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanacheza kwa malengo sawa.
Upande wa mashabiki Austin amewarai mashabiki kufika uwanjani mapema, amefurahishwa na njaa ya mashabiki ya kutaka kuja kuishabikia timu ya taifa na ameahidi kuwa atawapa burudani.
Kuhusu umuhimu wa mashindano haya, Austin Odhiambo amesema kuwa hii ni nafasi ya pekee kwa wachezaji kuionyesha dunia uwezo wao. Itakuwa nafasi ya kipekee ya kufungua milango ya wachezaji wengi kuenda kucheza ughaibuni.
Kenya itacheza dhidi ya DRC Congo kwenye mchuano wao wa kwanza ugani Kasarani kuanzia saa 9 (Tisa) mchana hapo kesho.
Je, Una Hisia Gani?
Penda
1
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0