AFCON 2025: NIGERIA KULA UNONO
Nigeria watawazima Morocco mbele ya umati wao nyumbani?
Michuano ya AFCON 2025 ikielekea kipindi cha lala salama. Nigeria maarufu kama The Super Eagles ni mojawapo ya timu ambazo kiukweli zimewashangaza wengi, sio kwa kuwa timu mbovu bali kwa kuonyesha viwango vya hali ya juu kwenye mashindano haya. Baada ya kukosa kufuzu Dimba la Dunia wengi walitarajia kuwa wataboronga kwenye michuano hii.
Chini ya mkufunzi Eric Chelle Nigeria wako nusu fainali na wanatarajiwa kucheza na wenyeji Morocco siku ya kesho na ni mojawapo ya michuano ambayo Dunia imesubiri kwa hamu. Mashabiki kote Duniani wanataka kuona ni kipi kimeandaliwa na pande zote mbili, wote wana wachezaji tajika ambao wanacheza Ligi bora Duniani.
Kwa Nigeria hatuezi sema wana shinikizo, shinikizo liko kwa mwenyeji Morocco ambaye kuupoteza mchuano huu itakuwa ni chumvi kwenye kidonda na aibu mbele ya mashabiki wake ambao wako nyumbani. Kwenye kambi ya Nigeria nao wakipiga hatua watakula unono, Bilionea Abdul Samad Rabiu amewaahidi dola laki tano (500,000) na Dola elfu 50,000 kwa kila goli ambalo watafunga dhidi ya Morocco. Ameongeza kuwa yuko tayari kutoa Dola milioni moja ikiwa The Super Eagles watatwaa ubingwa wa AFCON 2025 na Dola Laki moja (100,000) kwa kila bao ambalo watafunga kwenye fainali.
Unadhani Nigeria watatumia ahadi hii kuwanyamazisha Morocco ya kutwaa ubingwa mwaka huu na kuzima ndoto yao ya kusubiri ubingwa huu kutoka 1976?
Je, Una Hisia Gani?
Penda
0
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0