USICHOKIJUA KUHUSU MICHUANO YA CHAN
Michuano ya CHAN itaanza rasmi tarehe 2 Agosti 2025 na itakuwa ni mara ya kwanza kwenye historia Kenya, Uganda na Tanzania wanaaanda mashindano haya.
MICHUANO YA CHAN 2024
Kenya, Uganda na Tanzania ndio mkoko unaalika maua. Historia inasuburi. Itakuwa ni mara ya kwanza kabisa kwenye historia ya mataifa haya ya Afrika Mashariki kuandaa mashindano haya nna yataanza rasmi tarehe 2 Agosti mwaka huu na kukamilika tarehe 30 Agosti. Miji 4 itakuwa mwenyeji wa mashindano haya. Dar salaam na Zanzibar City (Tanzania) Nairobi (Kenya) na Kampala (Uganda).
Mashindano haya yalianza rasmi 2009. Kumekuwa na Makala 7 na mashindano ya mwaka huu yatakuwa ni makala ya 8.
Jumla ya mataifa 19 yatashiriki mashindano ya CHAN 2024, idadi kubwa zaidi kuwahi kushiriki kwenye historia ya mashindano haya.
Bingwa wa mashindano haya ya CHAN 2024 atashinda jumla ya Dola milioni 3.5 hii ni sawa na Ksh. Milioni 452.2, nafasi ya pili watapokea Dola Milioni 1.2 (KSH. 258.4 milioni) wanapokea laki 7 (KSH. 90.4Milioni) na wane wanapokea laki 6 (KSH. 77.5 Milioni)
Kenya na Central Africa Republic zitakuwa zinashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza kwenye historia. Uganda na DRC Congo ndio mataifa ambayo yameshiriki fainali ya mashindano haya mara nyingi Zaidi.
DRC Congo na Morocco ndio mataifa pekee yameshinda CHAN mara 2. DRC Congo ni bingwa wa 2009 na 2016 huku Morocco wakitwaa ubingwa 2018 na 2020.
Je, Una Hisia Gani?
Penda
1
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0