CAF WAMEUPITA MTIHANI WA AFCON 2025
Mashindano ya mwaka huu yamekuwa ya faida sana kwa shirikisho la soka barani Africa.
Wengi wanasema kuwa mashindano ya mwaka huu nchini Morocco yalikuwa ya aina yake na hakujawahi kuwa na mashindano kama haya kwenye historia ya AFCON ila kwa wengine ya mwaka huu imekosa msisimko ambao tumezoea kwenye mashindano haya. Huu ni mjadala ambao hautaisha.
Wenyeji Morocco wamefika fainali na watapambana na miamba wa soka barani Afrika Senegal kwenye uga wa Prince Moulay Abdellah Stadium, siku ya Jumapili tarehe 18, Januari 2026, Saa nne usiku.
Wadadavuzi wanasema kuwa jumla ya mashabiki milioni 1,234,693 wamehudhuria mashindano haya kufikia hatua ya nusu fainali na tayari imepita idadi ya Milioni 1.1 ya waliohudhuria AFCON 2023 nchini Ivory Coast.
Kwenye hatua ya makundi pekee mashabiki laki 729,240 walienda viwanjani kushabikia mataifa yao huku mchuano wa Morocco dhidi ya Nigeria ukirekodi mashabiki wengi kwenye mashindano haya ya mwaka huu, jumla ua mashabiki 65,458 walihudhuria mchuano huo.
Kwenye upande wa hela CAF inasema kuwa mashindano ya mwaka huu yamekuwa ya faida na wameweza kuwa na faida ya hadi asilimia 90% huku udhamini ukifikia dola milioni126, mashindano ya mwaka huu ina wadhamini 23 na hii ni rekodi ya juu kuwahi kutokea kwa mashindano haya, haki za matangazo iliongezeka, tiketi ziliongezeka. Faida halisi kwa CAF inatarajiwa kuwa karibu dola milioni 114. Mshindi wa AFCON 2025 atapokea dola milioni 10.
Michuano ya AFCON inatazamwa na mashabiki wa soka kote duniani. Huku kukiwa na chaneli zaidi ya 20 ambazo zinaonyesha mashindano haya barani Uropa huku kukiwa na jumla ya zaidi ya Chaneli 180 zinazopeperusha mashindano haya duniani. Hii ina maana kuwa zaidi ya mashabiki Bilioni 1.5 kote duniani wanafuati burudani hili la AFCON.
Mashindano yakitamatika hapo kesho unadhani nani atakuwa bingwa, ni Terenga Lions ama Atlas Lions?
#AFCON2025 #Africa
Je, Una Hisia Gani?
Penda
1
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0