GOR MAHIA WATAWEZANA NA MAKALI YA POSTA RANGERS?
Posta Rangers wako kileleni mwa jedwali Ligi Kuu nchini, unadhani wataendelea kubaki hapo ama mambo yatakuwa magumu leo?
Posta Rangers wameanza msimu huu kwa kasi sana, wana alama 10 baada ya kucheza mechi 4 kwenye Ligi Kuu ya soka nchini. Wameshinda mechi 3 na kutoka sare mechi 1. Walianza na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mathare United, 2-1 dhidi ya wanamvinyo Tusker, wakapiga sare ya 2-2 dhidi ya AFC Leopards na kuwapigia Shabana nyumbani kwao 2-1 kabla ya kwenda kwenye michuano ya kimataifa.
Leo watakuwa na mtihani mgumu dhidi ya Gor Mahia ambao wana kiu pia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mchini msimu huu na wana alama 6 kutoka kwa mechi 3 ambazo wamecheza. Walipoteza mchuano wao wa kwanza dhidi ya Bidco United na wakaandikisha ushindi dhidi ya Batoto ba Mungu Sofapaka na wanabenki KCB.
Mara ya mwisho timu hizi zimekutana Gor Mahia waliandikisha ushindi na kwenye michuano ya awali ambayo timu hizi zimekutana kichapo kikubwa cha Gor Mahia kwa Wanaposta ilikuwa ni kichapo cha 5-0 Julai 2018.
Mkufunzi wa Posta Rangers Sammy Omollo anaonekana kukisuka kikosi chake vyema msimu na kwenye hizi mechi 4 ambazo wamecheza zote wamefunga magoli mawili kwenye kila mchuano. Mshambuliaji wa Posta Rangers Eliud Lokuwam tayari amecheka na wavu mara 2 msimu huu, sawa na Trevor Omondi ambaye pia amebisha mlango mara 2 na ukafunguka.
Unadhani huu utakuwa wakati bora wa kuizima Gor Mahia na kulipiza kisasi?
Mechi zingine za Ligi Kuu ni:
Shabana FC vs Mathare United (2PM)
Murangá Seal vs Tusker FC (3PM)
Je, Una Hisia Gani?
Penda
0
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0