BLUE SHARKS WA CAPE VERDE WATAWEKA HISTORIA?

Cape Verde wanahitaji tu ushindi kwenye mchuano wa leo dhidi ya Eswatini Kufuzu Dimba la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye historia.

Oct 13, 2025 - 14:53
 0  5
BLUE SHARKS WA CAPE VERDE WATAWEKA HISTORIA?
Mashabiki wa Cape Verde kwenye mchuano wao wa awali.
BLUE SHARKS WA CAPE VERDE WATAWEKA HISTORIA?

HISTORIA inaisubiri bara la Afrika leo usiku. 

Cape Verde watafuzu michuano ya 2026 FIFA World Cup ikiwa wataandikisha ushindi dhidi ya Eswatini ambao hawajashinda mchuano wowote kutoka 2022. Vile vile watafuzu ikiwa Cameroon ambao ni wa pili kundi hilo watashindwa kuwapiga Angola. Ikiwa The Blue Sharks watafuzu watakuwa taifa la pili ndogo kufuzu dimba la Dunia baada ya Iceland kuwa taifa la kwanza ndogo kufuzu mashindano haya. Nchi ya Cape Verde ina takriban watu laki 5. 

Watakuwa pia taifa ndogo kwenye historia kutoka bara la Afrika kuwahi kufuzu Dimba la Dunia. Cape Verde wanaongoza kundi D ambalo lina Cameroon, Libya, Angola, Mauritius na Eswatini. Baada ya kucheza mechi 9, wana alama 20, wameshinda mechi 6, kutoka sare mechi 2 na kupoteza mechi 1. Hili ni kundi ambalo wakati lilitangazwa wengi walijua itakuwa kazi rahisi kwa Cameroon na Angola lakini mpira wa Afrika umebadilika sana hakuna mnyonge dakika 90 uwanjani zinaamua nani atashinda kila siku ni mwendo wa mende kuangusha kabati.

Cameroon ambao wanatarajia miujiza na kuomba Cape Verde ipokee kichapo kutoka kwa mpinzani wake wa leo wako nafasi ya pili na wana alama 18. Safari yao haitaishia hapa ikiwa watashinda na wakose kufuzu moja kwa moja bado wako nafasi ya kuenda kushiriki michuano ya michujo itakayo husisha timu bora 4 zilizomaliza nafasi ya 2 kutoka bara Afrika na zitamenyana na maitaifa ya mabara ingine. 

Mataifa mengine ya Afrika ambayo yana matumaini ya kufuzu kwa mara ya kwanza kabisa ni Benin ambao watacheza mchuano wao wa mwisho hapo kesho dhidi ya Nigeria. Gabon ambayo wako kundi moja na Kenya, watacheza mchuano wao wa mwisho dhidi ya Burundi huku wakipiga hesabu za Kenya kuwaharibia Ivory Coast sherehe wakiwa ugenini. Mataifa mengine ya Afrika ambayo tayari wamefuzu ni Tunisia, Egypt,Algeria, Morocco na Ghana. 

Ungependa kuona nani anafuzu kombe la Dunia kutoka barani Afrika?

Je, Una Hisia Gani?

Penda Penda 1
Sipendi Sipendi 0
Penda Penda 0
Ya Kufurahisha Ya Kufurahisha 0
Mwenye hasira Mwenye hasira 0
Huzuni Huzuni 0
Lo! Lo! 0