MASHETANI WEKUNDU WAMEKWARUZA CHELSEA.
UNITED LEO HANA MASIHARA AMEKUJA KUMALIZA
Mashetani Wekundi Manchester United wamewakwaruza Chelsea ugani Old Trafford na kubeba alama zote 3. Mechi ilianza kwa kasi na pande zote mbili zilishuhudia kadi nyekundu. Dakika ya 5 kipa wa Chelsea Robert Sanchez alimnyima Bryan Mbeumo nafasi ya kufunga na akapokea kadi Nyekundu. Shinikizo kutoka kwa United iliendelea na dakika ya 14 United walifunga bao lao ia kwanza kupitia nahodha wao Bruno Fernandes.
Dakika ya 17 Casemiro alipokea kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Enzo Fernandez. Dakika ya 37 Casemiro aliwapa Manchester United bao la pili na dakika 8 baadaye akapokea kadi ya pili ya njano kwa kumvuta Andrey Santos.
Kipindi cha pili kilishuhudia tu bao moja na lilikuwa la Chelsea la kuvutia machozi na lilifungwa na Trevoh Chalobah. Manchester United wamepanda hadi nafasi ya 10 na alama 7 huku Chelsea wakiwa nafasi ya sita na alama 8.
Je, Una Hisia Gani?
Penda
0
Sipendi
0
Penda
0
Ya Kufurahisha
0
Mwenye hasira
0
Huzuni
0
Lo!
0